GET /api/v0.1/hansard/entries/1526699/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1526699,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1526699/?format=api",
    "text_counter": 171,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, naelekea hapo. Nilikuwa naweka msingi thabithi ndiyo niweze kuuliza swali langu. Najenga hoja. Swali ambalo ningetaka kuuliza ni moja, katika takwimu ambazo umeleta hapa ukasema kwamba makadamia ilipouzwa ikiwa na maganda ilikuwa inaleta takriban shilingi 121 na ikiongezewa thamana ilikuwa inatoka shilingi 816. Ilikuwaje basi wakati ilikuwa inatoka shilingi 816 wakulima walikuwa wanapata shilingi 30 pekee? Wakati huo ilibidi Waziri aliyeondoka, Bw. Linturi, kuondoa makataa ile yaliyokuwepo ndiyo wakulima wauze makadamia ikiwa na maganda? Soko ni mbili, kuna makadamia iliyowekwa thamana na ambayo haijawekwa thamana. Hii ni kusema ya kwamba tuuwe ile soko ambayo inanunua makadamia ambayo iko na maganda kwa ajili ya ile ambayo iko nchini. Je, bei ikiteremka, itakuwaje? Hii ndio maana nilikuwa naomwomba Bw. Waziri uweze kutafuta wakati tuzungumze. Wakati mlitoa makataa, mimi mwenyewe nilikuwa nimeuza makadamia yangu katika bei ya shilingi 150."
}