GET /api/v0.1/hansard/entries/1526712/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1526712,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1526712/?format=api",
    "text_counter": 184,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Nadhani Bw. Waziri amekazana kujibu maswali yote. Hata hivyo, amesema tunafaa tuendelee na mazungumzo. Bw. Waziri, mimi ningesema hivi kwa ufupi, uchukue nafasi uweze kutembelea wale watu ambao wanauza makadamia kutoka nje ili uangalie hata kama ni quota system kama inaweza enda. Pia nikuambie kama mkulima, bei tayari imeshuka. Niliuza makadamia kwa shilingi 150 na ninaongea kwa niaba ya wakulima wote wa makadamia. Saa hii hata nikipeleka na ninahitaji shilingi 80 siwezi kununuliwa. Wakulima wamejaza maghala yao na makadamia kwa sababu marufuku ya kuja wakati wanavuna. Itakuwa ni vizuri zaidi ikiwa huo msongamano utaondolewa ili makadamia ambayo ilikuwa imenunuliwa halafu tuendelee na hiyo nyingine. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}