GET /api/v0.1/hansard/entries/1526741/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1526741,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1526741/?format=api",
"text_counter": 213,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murang’o",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Ni vizuri ijulikane kwamba pia Sen. Wakili Sigei ni mkulima wa majani chai na ndiye amedhamini Mswada ulioko mbele yetu wa kudhibiti majani chai. Sijui kama yake ni kama yangu ama ni namna gani? Bw. Spika wa Muda, mambo tunayosema ya kufungua soko ni magumu, lakini nyoka angeficha sumu yake, watu wengi wangemtumia kamba. Kwa hivyo, toa sumu kidogo ili wakulima waweze kufaidika. Wakulima wamebaki kula makombo kwa sababu ya wakiritimba na wale wanajiita waongeza thamani waliopo katikati. Kwa hivyo, siuzi makadamia katika soko ya nje, bali mahali wakulima wanauza. Nimeuza tani hamsini ya makadamia juzi. Kwa hivyo, ninapoongea naongea kwa niaba ya yule mkulima mdogo ambaye yuko na miti mitatu ambaye hawezi fika hapa akajitetea mbele ya Bw. Waziri. Naongea kwa niaba ya wakulima wanaoishi katika milima ya Nyambene kule Meru ambao hawawezi kuteremka mlima kuja mpaka Nairobi kujiwakilisha. Kwa hivyo, ninaposimama hapa, nitatetea wavuvi, wakulima, wafugaji na wote kwa sababu sisi sote ni Wakenya. Tunapoondoa ukabila, tuondoe na ubaguzi wa wakulima. Kama sheria ipo, inafaa iwe kwa mkulima wa mahindi, korosho na makadamia. Ibara 53 inayosema makadamia iuziwe bwenyenye ili iongezwe thamana ni kandamizi mkulima wa kawaida. Sheria siyo nzuri kwa watu wetu. Asante sana, Bw. Spika wa Muda."
}