GET /api/v0.1/hansard/entries/1526766/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1526766,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1526766/?format=api",
"text_counter": 238,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Bw. Waziri, pongezi kwa sababu ulikuwa Waziri wa Afya katika Serikali iliyopita na ukafanya kazi nzuri. Vile vile, katika Serikali ya muungano ya Kenya Kwanza, umekuwa Waziri wa Kilimo. Mimi ni Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Agriculture and Livestock Development. Mkishirikiana na AFA, kazi na mipango na mliyo nayo kwa mkulima wa makadamia sio mbaya. AFA ya zamani haikuwa ifanya kazi vile inafaa lakini siku hizi inafanya kazi nzuri. Tunajua makadamia ilikuwa inatoka shilingi 200 kwa kilo moja hapo awali. Wakati Serikali hii ilipoingia ikawa inauzwa kwa shilingi 30. Hata hivyo, Serikali ilisikia kilio na ikaongezea muda wa barua mwaka moja ili makadamia ikauzwa kwa shilingi 120. Muda huo ulipoisha, mwezi wa Novemba, tuliongea na Bw. Waziri aliyekuwapo ambaye alitemwa, aongezee miezi sita ili kamati ya Agriculture and Livestock Development na kaunti zile zingine wakae chini tuone vile mkulima na manufacturers watafaidka kwa sababu mnasema kwa muda wa miaka mitatu makadamia ya Kenya haitaenda nchi za ng’ambo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}