GET /api/v0.1/hansard/entries/1527453/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1527453,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1527453/?format=api",
    "text_counter": 209,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante sana, Bw. Spika kwa kunipa fursa hii, kuunga mkono Mswada wa makavazi na utamaduni. Huu ni Mswada wa Seneti na umewasilishwa bungeni na mwenyekiti wa Kamati ya Leba na Ustawi wa Jamii. Nilihudumu katika kamati hii kwa muda wa miaka miwili na nusu iliyopita. Nimesoma Mswada huu. Yale mambo yanayozungumziwa yatasaidia pakubwa kuweza kukinga na kuhifadhi utamaduni na mila zetu nchini. Mambo ya utamaduni na makavazi yamegatuliwa kulingana na Ibara ya nne ya Katiba yetu. Ule Mswada kwa sasa ambao ni sharia - Mswada wa Makavazi na Utamaduni wa mwaka 2006 umepitwa na wakati kwa sababu kulingana na Katiba mpya tuko katika himaya ya Serikali mbili- ya kitaifa na za ugatuzi. Bw. Spika, ni muhimu Mswada huu uweze kuangilia sehemu zote mbili. Kaunti zetu nyingi mpaka sasa hazijaweza kutenga fedha za kutosha kuhakikisha kwamba wanasimamia makavazi tofauti tofauti katika maeneo yao na vile vile kusimamia mambo ya mila na tamaduni katika maeneo wanakotoka. Kwa mfano, katika kaunti ya Mombasa, hatujaona bajeti au mradi wowote wa makavazi katika maeneo hii ambayo inasimamiwa na kaunti zetu. Tukiangalia sehemu zingine kama Kaunti ya Kilifi, kuna kaya zetu ambazo watu wamekuwa wanaenda kwa muda mrefu kumwomba Mungu na vile vile kufanya matambiko yao ya kitamaduni. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}