GET /api/v0.1/hansard/entries/1527454/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1527454,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1527454/?format=api",
    "text_counter": 210,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Fedha ambazo ziko ni kidogo na pia hakukuwa na sheria ambazo zingesimamia mambo kama hayo. Mswada huu utasaidia pakubwa kuhakikisha kwamba serikali zetu za kaunti zinaweza kuangalia swala hili muhimu katika maisha ya binadamu. Vile vile katika usimamizi wa makavazi utapata kwamba zile sehemu zote za kihistoria kwa mfano Fort Jesus na Mama Ngina Water Front amabayo ilikarabatiwa majuzi na serikali kuu katika Kaunti ya Mombasa hazijapewa hati miliki ya makavazi na serikali kuu. Mara ya mwisho Waziri Miano alipozuru pale alisema kuwa ataliangalia swala hilo lakini juzi nilipomuuliza aliniambia kuwa swala hilo na mengine ya utamaduni yani heritage yametolewa kutoka Wizara ya Utalii na Wanyama Pori na limepelekwa na Ofisi ya Wizara ya Youth Affairs, Creative Economy and Sports . Bw. Spika naunga mkono Mswada huu na ukipitshwa utasaidia pakubwa serikali zetu za ugatuzi kuhakikisha kwamba wanachangia pakubwa kuhifadhi na kujenga turadhi zetu na vile vile makavazi yetu ya awali. Asante."
}