GET /api/v0.1/hansard/entries/1527667/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1527667,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1527667/?format=api",
    "text_counter": 71,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuchangia taarifa iliyowasilishwa na Sen. Mundigi kuhusu Hazina ya Afya. Wazee wengi ambao wamefikisha umri wa miaka 70 wanaishi kwa hali ya uchochole na umaskini. Kwa hivyo, naunga mkono ya kwamba Kamati itakapokuwa ikishughulikia jambo hili ishughulikie kwa dharura ili wananchi wa Kenya au wazee wetu ambao ni wakongwe waweze kulipiwa hazina ya afya na serikali, kwa sababu hata yale malipo ya uzeeni wakongwe wanapaswa kupatiwa inakuwa ni vigumu sana kwao kupata. Wanakaa miezi mingi bila kulipwa, ilhali hao wazee ni rahisi sana kupata magonjwa kwa sababu unapoendelea kukua kwa miaka, huwezi kukosa kupata magonjwa. Kila wakati wana madawa ambayo hata kuyanunua ni kazi ngumu. Si hao tu. Pia walemavu wanapata shida nyingi kwa sababu hata kupata ajira kwao ni vigumu sana. Katika gatuzi zetu imesemakana kuwa asilimia fulani inapaswa kutengewa walemavu lakini unapata hiyo haitendeki. Hata Serikali Kuu haiwaajiri walemavu. Kwa hivyo, ni vizuri Kamati itakapokuwa ikishughulikia jambo hili iangalie kwa kindani wakongwe wetu pamoja na walemavu washughulikiwe. Naunga mkono taarifa iliyotolewa na Sen. (Prof.) Ojienda kuhusu reli kupelekwa moja kwa moja hadi Kisumu, hata mpaka Malaba, mahali mpaka wa Kenya na Uganda uliopo. Hiyo itaongeza biashara. Watu wataweza kusafiri kwa urahisi. Mahali ambapo reli itapitia katika nchi yetu ya Kenya, biashara zitaimarika na wale wengine ambao walifikiria sehemu zao ni kama zimewachwa zitafunguliwa reli itakapopitia hapo na watu wengi watanufaika. Nashukuru."
}