GET /api/v0.1/hansard/entries/1527670/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1527670,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1527670/?format=api",
    "text_counter": 74,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "mtungi wa gesi na kichwa ambacho kinawaka moto unafaa kubadilishwa baada ya miaka miwili. Lakini, utapata wengine wanatumia ile ile tangu waliponunua mtungi huo. Mara nyingi, hiyo pipe huwa inalika ndani na ikilika inasababisha gesi kuvuja. Ikivuja, inasababisha mlipuko ama moto kwa urahisi. Kwa hivyo, jukumu hili la kupambana na moto pamoja na dharura nyingine ni jukumu la kaunti zetu. Ni lazima kaunti zetu zikishirikiane na Energy and Petroleum Regulatory Authority (EPRA) na wahudumu wa wazima moto waanzishe mikakati ya kuwaelimisha wananchi juu ya matumizi ya gesi kwa sababu mara nyingi wengi wanatumia gesi hizo bila elimu yoyote na inawafanya kuingia katika hatari ambayo ingeweza kuepukika. Kwa mfano, katika Kaunti ya Mombasa, nyumba moja ya Kiswahili ina room karibu kumi na kila mtu ana meko. Kwa hivyo ikilipuka, utapata milipuko kumi kwa wakati mmoja kwa sababu ule moto unasambaa kwa haraka na vile vile inakuwa ni hatari kwa binadamu na kwa raslimali ama majumba ya watu wao. Asante."
}