GET /api/v0.1/hansard/entries/153086/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 153086,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/153086/?format=api",
"text_counter": 343,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ms. S. Abdalla",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 380,
"legal_name": "Shakila Abdalla",
"slug": "shakila-abdalla"
},
"content": "Asante sana Bi. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii kuchangia Hoja hii muhimu sana. Nitachukua nafasi hii kumpongeza Bw. Wamalwa kwa kuleta Hoja hii ya kuwatetea wale waliohamishwa kwenye mashamba yao na ardhi yao. Hakika, ni jambo la kusikitisha sana kwamba hata ukiangalia kwenye kamusi ya Kiswahili, hakuna neno âskwotaâ. Kwa hivyo tunashangaa hili neno âskwotaâ lilitoka wapi? Ni hali ambayo tulibandikwa na Wazungu na tukaibeba, kumalizana wenyewe kwa wenyewe. Kwa hivyo, neno hilo halipo katika kamusi ya Kiswahili. Iliyoko ni kwamba, kuna watu waliohamishwa kwenye mashamba yao na ardhi yao. Jambo lingine ni kwamba Serikali hata kama itatenga pesa kwa kusaidia waliohamishwa kwenye ardhi yao---"
}