GET /api/v0.1/hansard/entries/153091/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 153091,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/153091/?format=api",
"text_counter": 348,
"type": "speech",
"speaker_name": "May 20, 2009 PARLIAMENTARY DEBATES 638 Ms. S. Abdalla",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ahsante sana mhe. Naibu Spika wa Muda. Ijapokuwa Serikali itatenga kiasi fulani cha fedha kuwahamisha wale waliofurushwa kutoka katika mashamba yao hadi mahali pengine, ni muhimu iweke sera kamili ya ugawaji wa ardhi kwa sababu hivi sasa, anayeweza kumiliki ardhi ni yule mwenye fedha, tajiri anayejimudu, mfanya biashara, mwanasiasa ama kiongozi fulani. Lakini mwananchi wa kawaida na watu wengi hawana uwezo wa kumiliki ardhi. Na hilo pia ni jambo ambalo tulibandikwa! Sisi Wakenya na Waafrika kutoka kila sehemu ni wenyeji kwenye ardhi zetu; hakuna mgeni. Lakini wageni walikuja wakanyakua ardhi na sisi tukaishia kuwa wageni. Wao wakawa wenyeji kwa sababu ya umilikaji wa ardhi na hivyo vyeti vya kumiliki ardhi! Kwa hivyo, ni muhimu Serikali iweke sera na mwelekeo wa ugawaji wa ardhi ambao utanufaisha kila mwananchi. Uhamishaji utazidi kuendelea ikiwa watu hawatamilikishwa ardhi zao! Wizara ya Ardhi ichukue jukumu lake kikamilifu kwa kutogawia watu ardhi kiholela! Kuna watu wanagawiwa ardhi kiholela. Bi. Naibu Spika wa Muda, hivi sasa, kuna mradi mkubwa unaokuja Lamu wa bandari. Sisi wenyeji wa Lamu tunahofia sana kuwa tutaishia kuwa maskwota ikiwa hatutamilikishwa ardhi zetu mapema kabla ya huo mradi. Kwa hivyo, ni muhimu pesa zitengwe za kuwawezesha watu kupatiwa nafasi za kumiliki ardhi sehemu zingine. Lakini pia, ni muhimu kwa Serikali kuweka mipango kamili ya watu kumilikishwa ardhi wanamoishi. Ni lazima Wizara ya Ardhi ichukue jukumu lake na iwache kugawa ardhi nyingi kiholela kwa watu wanaojiweza, ili kuwadhulumu wale wanaoishi katika ardhi hizo. Hivi sasa, kuna mambo mengi sana yanayoendelea! Watu wanapewa ardhi kubwa kubwa, kiholela, na watu wapo ndani. Je, hao wenye kupeana hizo hati za kumilikisha ardhi wale wanaojiweza, wana mipango gani kwa wale ambao wako kwenye hizo ardhi? Kwa hivyo, haitoshi pesa tu kutengwa na watu kuendelea kuhamishwa kutoka kwenye ardhi zao. Mpango huo ni sawa. Tunakubaliana nao kwa sababu ni jambo liko na limeanza. Lakini mipango kamili iwekwe ya watu kuwamilikishwa watu ardhi zao kabla hawajahamishwa na wale wanaojiweza. Hatutaki isemekane kwamba wataenda kupewa hizo pesa zilizotengwa na Serikali ili wamilikishwe ardhi sehemu zingine. Bi. Naibu Spika wa Muda, sina mengi ya kusema. Naomba kuunga mkono Hoja hii. Ahsante."
}