GET /api/v0.1/hansard/entries/153119/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 153119,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/153119/?format=api",
    "text_counter": 376,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Joho",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 30,
        "legal_name": "Hassan Ali Joho",
        "slug": "hassan-joho"
    },
    "content": "Nimepata ujumbe kutoka kwa maskwota wangu nikiwa hapa. Hii ni kwa sababu niko hapa kwa sababu ya maskwota. Asilimia 80 ya watu katika Wakilisho langu ni maskwota. Maoni yanayotolewa ni kwamba huu ni muundo wa Serikali. Ni ulegevu na ubinafsi wa Serikali iliyotangulia na ile iliyofuata. Kwa hivyo, tunawajibika kama Bunge kuweka mikakati kabambe ya kulitatua hili suala. Hakuna mtu aliyekuja hapa na ardhi. Hata mzungu aliipata ardhi hapa. Kule kwetu Kisauni, kuna eneo kubwa la makazi ambalo tunataka kugawanya lakini hatuwezi. Hii ni kwa sababu kuna mtu mmoja ambaye alikuwa Waziri ambaye amechukua kipande kikubwa cha ardhi katikati mwa eneo hilo. Hatuwezi kugawanya ardhi hiyo mpaka kipande hicho cha ardhi kinunuliwe. Yeye anatumia utawala kujikinga. Kwa hivyo Serikali hii inakupatia kwa mkono wa kulia na kuchukuwa kwa kutumia mkono wa kushoto."
}