GET /api/v0.1/hansard/entries/1532629/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1532629,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1532629/?format=api",
"text_counter": 4882,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": "Leo tumeona Mswada huu ambao tumeusubiri sana. Kwanza, twauunga mkono. Kando na kuunga mkono, tumeona kuwa hii Supplementary Estimates II ama Bajeti ya Nyongeza imejumuisha vitu vyingi sana vya maana. Zaidi, nitasema kama mwanasiasa. Kila zinapotengenezwa, Bajeti hizi huangalia ni namna gani zitaweka mwelekeo wa kisiasa ili kukimu na kuzingatia yale wananchi wanataka kuona. Leo, Bajeti hii imetenga fedha za humansettlement. Yaani, za makao ya binadamu. Wako akina mama wasio na makao. Mfano ni mama Lydia, aliyekuja kunililia wiki iliyopita. Leo, pesa hizi za human settlement zitatusaidia mahali ambapo watu wamepangiwa kuondolewa. Mifano ni kama Kwa Punda, Alidina, Vikobani, Owino-Uhuru, Kibarani na sehemu nyingine nyingi katika eneo bunge langu. Mhe. Rais alikuwa Mombasa wiki iliyopita. Alituhakikishia kuwa wataweka pesa ili mabwenyenye ama wanaowasumbua wananchi waone kuwa serikali inaweza kuwafidia ili wapimie wananchi ardhi. Tunamshukuru Mhe. William Ruto kwa kujali maslahi ya wananchi ili wapate mahali pa makao. Vilevile, twaona pesa za State House Affairs ni kidogo katika Bajeti hii—ni kama Ksh 6 ama Ksh7 milioni. Hii inaonyesha kuwa State House imekataa mambo ya ubadhirifu. Ndio The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}