GET /api/v0.1/hansard/entries/1532632/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1532632,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1532632/?format=api",
    "text_counter": 4885,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": "ambazo ni magereza, kwa Ksh34 milioni. Ningependa kutoa pendekezo langu katika sehemu hii kama Mbunge wa Jomvu. Tufuate afanyavyo Rais Ibrahim Traore wa Burkina Faso. Hivi sasa twaongeza pesa za walio gerezani kwa Ksh34 milioni. Twawalisha na wanalala bure. Siku hizi tumewawekea hata televisheni na wanacheza michezo bure. Hivi sasa, katika masuala haya, ni muhimu wafungwa hawa watolewe wakafanye ukulima katika viwanja ama ardhi za serikali ambazo hazitumiki ili waongeze thamani nchini, na vilevile kutuwezesha kukabiliana na njaa kwa njia nzuri."
}