GET /api/v0.1/hansard/entries/1532637/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1532637,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1532637/?format=api",
"text_counter": 4890,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": "Kuna pesa ambazo zimewekwa za mabarabara. Kila mnenaji hapa amesema kuwa jukumu la kwanza la mambo haya ni barabara zilizosimama. Kule kwangu kuna barabara ambayo nimeipigia kelele sana, ya Jitoni-Rabai, ambayo kuna kipande kidogo cha mita 800 ambacho hakijakwisha. Namshukuru Rais kwa sababu juzi alipokuwa Coast, alisema hali hiyo itaweza kuangaziwa. Nikiwa mwanakamati wa barabara, nilikaa katika kamati yangu na Waziri Davis Chirchir, ambapo alisema jambo hili litaweza kutiliwa maanani na kuona kuwa kipande hicho kitamalizwa. Jambo kama hili nampa shukrani na pongezi nyingi sana Waziri wetu wa barabara. Aliweza kuangalia bajeti za nyuma nakuona, kama wanenaji walivyosema hapa, ya kwamba kuna sehemu moja imewekewa mabilioni, na kuna kaunti nzima imewekewa Ksh215 milioni, ilhali pia kuna sub-county ina Ksh5 bilioni ama Ksh6 bilioni. Hii sio hali njema ya Kamati kufanya kazi. Kamati ikipewa nafasi kufanya kazi, ijue haiwezi kuhudumia maeneo bunge ya wanakamati pekee yake. Imepewa kazi ya kuhudumikia eneo la Kenya nzima. Kwa maana hiyo, namshukuru sana Waziri wetu, Bw. Davis Chirchir, kwa kutumia Article 223 yaKatiba kuhakikisha kuwa kuna usawa katika kila sehemu na barabara zimeguswa."
}