GET /api/v0.1/hansard/entries/1532638/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1532638,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1532638/?format=api",
"text_counter": 4891,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": "Kwa hivyo, hata wanakamati ambao wanaingia sasa, wasifuate mtindo huo. Watakaofuata mtindo huo wakijiona wanajitengenezea watakuwa wakimharibia Rais ambaye alipigiwa kura na Kenya nzima. Ndiyo maana nimeketi hapa kutoa shukrani na pongezi kwa dadangu, Irene Mayaka, kwa kuchaguliwa kama Chairlady wa Regional IntegrationCommittee . Yeye ni mwenyekiti na ameketi hapa mpaka saa hizi. Wenyekiti wengine washakwenda zao. Inafaa wakae hapa kila siku kama Irene Mayaka. Mambo ya barabara tunasema yataendelea. Kwangu Jomvu, barabara nyingi zimetengenezwa. Nikiangalia Mheshimiwa ambaye amezungumza hapo awali, alisema kwao hata 1 per cent hakuna. Leo utamkuta mtu akipiga kelele kwamba kipande chake cha mita 800 The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}