GET /api/v0.1/hansard/entries/1537571/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1537571,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1537571/?format=api",
"text_counter": 69,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Nimesimama kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu No.51(1) ya Kanuni za Bunge la Seneti kuomba kauli kutoka kwa Kamati ya Kawi kuhusu kupotea kwa nguvu za umeme katika Kaunti ya Mombasa na viunga vyake, hususani mwezi huu mtukufu wa Ramadhan. Kutoka mwanzo wa Mwezi huu wa tatu ambao unaenda sawia na mwezi mtukufu wa Ramadhan, jiji la Mombasa na viunga vyake limeshuhudia kupotea mara kwa mara nguvu za umeme. Hii imeadhiri pakubwa mipango ya ibada na biashara kwa wakazi ikizingatiwa kwamba mwezi huu waumini wengi wa dini ya Kiislamu wanahusika na ibada ya sala ya usiku inayojulikana kama Taraweeh . Vile vile, biashara huongezeka mwezi huu kwa sababu watu wengi huenda madukani baada ya sala za usiku. Hivyo basi kupotea huko kwa nguvu za umeme kumeadhiri pakubwa sala pamoja na biashara. Katika kauli hiyo kamati ileleze- (1) Chanzo cha kupotea kwa umeme mara kwa mara katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan na ichukue hatua zinazofaa ili kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma wanazostahili. (2) Iorodheshe hatua ambazo Serikali inachukua kusuluhisha tatizo la kukatika kwa umeme jijini Mombasa ikizingatiwa kuwa Waisilamu wanashindwa kutimiza maombi yao ya usiku na wafanya biashara wanapata hasara kutokana na ukosefu wa umeme. Asante."
}