GET /api/v0.1/hansard/entries/1537763/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1537763,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1537763/?format=api",
    "text_counter": 261,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Sen. Joyce Korir kwa kazi nzuri aliyofanya. Hakuna kitu hata kimoja kwa wakati huu ambacho kinazuia magavana wa kaunti zetu kuhakikisha kuwa kuna maktaba katika kila wadi katika kaunti zetu. Yote tisa, kumi ni ukweli. Nakubaliana na Sen. (Prof.) Kamar kuwa mwacha mila ni mtumwa. Vile alivyosema, ukisoma Kipengee cha tatu inamaanisha kwamba tutakuwa tunahifadhi desturi na mila zetu. Vile vile, ukiangalia Kipengee cha tano, kuna vile ambavyo ameeleza kinagaubaga kwamba kutakuwa na kamati itakayoshughulikia maktaba. Kwa hivyo, mambo hayatafanywa kiholela. Kuna watu ambao watapatiwa jukumu na kazi yao itakuwa kufuatilia na kuona kwamba kuna maktaba katika kaunti zetu. Wengi wamesema kwamba wengi wa vijana wetu hawajishughulishi na mambo ya masomo. Utapata mtu amezama kwenye simu yake ya rununu na mambo anayosoma hayawezi kudhibitishwa. Vitabu ambavyo viko katika maktaba zetu vimedhibitishwa na vinakubalika. Kwa hivyo, vijana wetu wanapotembelea maktaba zetu, watakuwa wanasoma mambo ya kuelimisha. Hayo ni mambo ambayo yamekaguliwa katika nchi yetu ya Kenya na kwa hivyo mila na desturi zetu zitakuwa zikizingatiwa. Vipindi vinavyonyeshwa katika televisheni zetu ni vile ambavyo vimeangaliwa na vinakubalika. Unapotumia simu ya rununu, utapata kuwa mambo ambayo wanasoma pale hayakubaliki. Mila zetu zinaendelea kuisha. Nakubaliana na viongozi wengine ambao wameongea mbele yangu kwamba itaendeleza ujuzi wa vijana wetu. Huo ni ujuzi ambao unafaa kwa sababu unawezapata ujuzi ambao haufai. Mswada huu unanuia kupatia kaunti zetu nguvu kamili. Waziri anayehusika na mambo ya masomo atahakikisha kwamba kuna maktaba katika sehemu zote. Ijapokuwa naupigia upato Mswada huu, naomba magavana wetu, hata kabla ya Mswada huu kupita, waangalie vipengee hivi na kuanza kutekeleza majukumu haya katika kaunti zetu. Nchi ambayo haina ujuzi au vijana wasiosoma ni nchi ambayo inaendelea kuwa na upungufu. Kwa hivyo, naunga mkono Mswada huu kuwa tunafaa kuwa na maktaba katika kaunti zetu. Ni vyema ieleweke na kuwekwa paruwanja. Naomba Sen. Korir aweze kuangalia"
}