GET /api/v0.1/hansard/entries/1537765/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1537765,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1537765/?format=api",
"text_counter": 263,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "zitapewa nafasi ipi katika maktaba zetu. Teknolojia inaendelea kuimarika na vitu vipya vinaendelea kuchipuka. Ukisoma kitabu kipya leo, utapata kuwa mambo mapya yametokea. Mtu akisoma kitabu in hardcopy na mwingine asome in soft copy, yule wa soft copy anapata vitu vipya kwa sababu uzinduzi unaendelea kufanyika kila siku. Sisi tunaendelea kupambana kule kwetu Laikipia. Ukienda mahali kama Rumuruti au Salama, pengine tumeweka pale maktaba kulingana na jinsi Sen. Korir angetaka. Kuna vitabu pale. Nilipokuwa katika chuo kikuu, ungepata kuwa makala ambayo lecturer anakuja nayo yalikuwa yametumika kufunza watu kwa zaidi ya miaka 18. Mambo yamebadilika ilhali sisi tunaendelea kusoma mambo hayo hayo. Ni vyema tujue jinsi tutapanga maktaba zetu tukizingatia usasa kwa sababu teknologia tayari imekuja na iko pamoja nasi. Unaweza tu kuketi na kusomewa kitabu na kuelewa badala ya kwenda kwenye maktaba. Kwa mfano, pengine kuna maktaba The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}