GET /api/v0.1/hansard/entries/1538430/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1538430,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1538430/?format=api",
    "text_counter": 214,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante. Naunga mkono kuongezwa kwa fedha hizi katika kitengo hiki cha kuangalia hali ya usalama. Tumeona hali ya usalama imekuwa mbaya, hasa kwa sisi wanawake. Juzi na jana, tumeona wanawake wengi wameuawa katika hali za kutatanisha. Ikiwa fedha hizi zitaongezwa, kitengo hiki kitaweza kujisaidia kupata usafiri, kwani mara nyingi kinakosa. Vilevile, katika kazi zao, kitahakikisha kuwa dhuluma zimepungua na watu wamepata haki zao. Fedha hizi zitawawezesha. Kwa hivyo, ni muhimu sana hizi fedha ziongezwe na zitumike ili wananchi wa Kenya wapate haki zao na tusione tena maafa na dhuluma za kutekwa nyara. Ahsante sana. Naunga mkono."
}