GET /api/v0.1/hansard/entries/1545032/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1545032,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545032/?format=api",
"text_counter": 82,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika kwa fursa hii. Ningependa kuchangia kwa ile Taarifa ya Seneta Joe Nyutu kutoka Murangá, kuhusu kifo cha yule Bi. Joyster Muchina. Kwanza, ninapeana rambirambi zangu kwa familia ya mwenda zake kwa kupoteza maisha yake kupitia mikono ya watenda kazi wetu wa usalama. Ni kinaya kuona wale maafisa wa polisi ambao wanafaa kutupea usalama kama wananchi ndio wako mstari wa mbele kutoa maisha ya binadamu wetu. Hatua ile ya maafisa wa polisi kujihusisha na maswala ambayo ni ya kigaidi inafanya wananchi wetu wanapoteza uhai na hio si sawa. Kwa hivyo, ninapeana ilani kali sana kwa maafisa watakaopatikana kwa swala hili. Bw. Spika, ninachukua fursa hii kuzungumzia kudorora kwa usalama pale Kaza Moyo eneo bunge la Kinango. Utapata maafisa wa usalama, hususan maafisa wa GSU, wanahangaisha wananchi wetu pale Kaza Moya kiholela. Wananchi wamepigwa vita na maafisa wetu wa usalama. Vile vile, wengine wamejeruhiwa na wengine kupoteza uhai wao kwa sababu ya swala la maafisa wa usalama kudhibiti usalama. Naomba Kamati ya Usalama ifanye kazi yake kwa undani sana. Afisa atakayepatikana na hatua yeyote, Kamati hii ichukue hatua kali na ishikane na lile shirika la Independent Policing Oversight Authority (IPOA) ili maafisa hao wa usalama wapelekwe kortini na waachishwe kazi. Hii itakua funzo kwa maafisa wa usalama wengine kuwa sio vyema mwananchi wa Kenya leo hii apoteze uhai wake kupitia kwa mikono ya maafisa hawa. Ninampongeza Seneta Joe Nyutu kwa kuleta taarifa hii hapa Bungeni na nina imani kwamba Kamati hii itafanya kazi ambayo itasaidia Wakenya wote na kuhakikisha kwamba hatua kali zimechukuliwa dhidi ya maafisa hawa wanaokosa nidhamu na kupoteza maisha ya wananchi wetu mikononi mwao."
}