GET /api/v0.1/hansard/entries/1545034/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1545034,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545034/?format=api",
"text_counter": 84,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia kwenye Kauli iliyoletwa Bungeni na Sen. Abass, Seneta wa Wajir. Amezungumzia masuala ya ugonjwa wa Kala-azar . Ugonjwa huu umeingia katika Kaunti za kaskazini. Wiki iliyopita tulizungumzia Kaunti ya Marsabit, hivi sasa tunazungumzia Kaunti ya Wajir. Zamani, afya haikuwa imegatuliwa. Ilikuwa ni shida kupata wataalamu wa kupambana na majanga kama haya kwa muda mfupi. Kaunti zetu hazijafanya mipango yoyote kuhusiana na magonjwa kama haya. Inakuaje ugonjwa unaingia, wananchi wanafariki, sio mmoja bali wawili watatu. Ripoti ya magazeti ilisema kuwa watu kadhaa wamepoteza maisha yao kwa sababu ya ugonjwa huu. Ni ugonjwa ambao unaweza kutibiwa na kuepukwa wakati wananchi watazingatia usafi ili kupambana na masuala kama haya. Ni muhimu Bunge hii iangalie ni vipi kaunti zinapambana na majanga. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}