GET /api/v0.1/hansard/entries/1545035/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1545035,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545035/?format=api",
"text_counter": 85,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Hakuna mandalizi kwenye kaunti ya kupambana na majanga kama haya ambayo yanatokea mara kwa mara na kupoteza Maisha ambayo tungeokoa. Tulipopambana na janga la COVID-19, kaunti nyingi zilijitayarisha na kujenga vyumba vya wagonjwa mahututi. Hivi sasa tunashikwa na magonjwa madogo madogo kama haya ambayo yanaweza kutibiwa na kuepukwa iwapo kaunti zetu zitakuwa imara katika kuangalia afya ya umma katika maeneo yao. Pia ningependa kutoa maoni yangu kuhusiana na Kauli ya Sen. Githuku, Seneta wa Lamu. Kauli ni kuhusiana na ulipaji wa ridhaa kwa watu wanaoadhiriwa na masuala ya kushambuliwa na wanyama pori katika maeneo yetu. Hili limekuwa ni donda sugu. Juzi tulipata fursa ya kukutana na waziri. Tumemwambia kuwa tungependa kupewa orodha ya wale ambao wamelipwa kuanzia mwaka wa 2020 mpaka leo ili tujue kama malipo yanatolewa kulingana na wale ambao waliumia zamani ama malipo yanalipwa kulingana na wale wanajua maofisa wanaolipa. Kuna watu wengi walioshambuliwa na wanyama na wengine wamefariki na familia zao hazijapata ridhaa. Wengine ni vilema na familia zao hazijapata ridhaa. Ni muhimu Waziri aweze kueleza na atoe ---"
}