GET /api/v0.1/hansard/entries/1545044/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1545044,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545044/?format=api",
    "text_counter": 94,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante Bw. Spika kwa fursa hii ili niweze kutilia pondo Kauli iliyoletwa na Seneta wa Murang’a, Sen. Joe Nyutu, kuhusiana na maafisa wa polisi ambao wametumia mamlaka yao vibaya. Pale kwetu kwenye Gatuzi la Mombasa, kuna mwanamke mmoja katika eneo la Likoni aliyepigwa risasi akiwa ndani ya nyumba yake. Tunaweza kutoa matukio ya kisanga hicho. Cha kushangaza ni kwamba mpaka sasa, hata baada ya kujua kuwa kulikuwa na utepetevu kwa upande wa askari yule, hakuna fidia ambayo imepeanwa kwa jamii, kufuatiliwa kwa jambo lile au anwani yoyote kuandikwa katika kituo cha polisi chochote. Mume wa mwendazake alienda katika kituo cha polisi akanyimwa nafasi ya kuandika taarifa ya kifo cha mke wake. Naendelea kutamaushwa na mazungumzo haya. Kuna maafisa wa polisi wanaopeana usalama katika Kituo cha Central Police kilichoko mita 100 kutoka Uwanja wa Makadara Grounds kule Mombasa. Cha kushangaza ni kwamba watoto wanaorandaranda mitaani walipiga wananchi mawe msimu huu wa Ramadhani, ilhali hakuna hatua yoyote ilichukuliwa hadi baada ya lisaa limoja. Hiyo inaashiria kwamba wananchi wa Kenya wako peke yao kwa sababu hakuna mtu wa kuwaangalia na kuwalinda. Nikimalizia, tunaelekea msimu wa mvua nyingi. Kwa hakika, alivyozungumza Seneta wa Lamu, ni kweli kwamba Serikali ya Kitaifa, serikali za magatuzi na hata The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}