GET /api/v0.1/hansard/entries/1545045/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1545045,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545045/?format=api",
"text_counter": 95,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "National Government Constituencies Development Fund (NG-CDF) bado zina pesa ya kusaidia waathiriwa. Kuna hazina hizi zote za pesa. Kwa nini watu wasikae pamoja? Rais ameonyesha mfano mzuri wa kuweka viongozi wote pamoja. Kwa nini tusishughulikie maeneo kama Links Road kule Nyali ambayo tunajua miaka nenda miaka rudi kwamba mvua inaponyesha kupita kiasi maji hayapiti? Kwa mfano, tunapozungumzia kuwatahadharisha wananchi kupitia kaunti, hatuzungumzii tu kuzibuliwa kwa njia za majitaka. Tunazungumzia pia wale watu watakaopeana huduma ya kwanza kupewa vifaa. Kwa kuwa tunajua kwamba maji mengi yanaingia katika maeneo fulani, tunafaa kuwa na shule ambazo zimetayarishwa kupokea waathiriwa wa majanga kama yale. Tunaomba sisi kama Seneti tusiwe---"
}