GET /api/v0.1/hansard/entries/1545073/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1545073,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545073/?format=api",
    "text_counter": 123,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Bw. Spika, nataka kuunga mkono Taarifa iliyotolewa hapa na ndugu yetu Sen. (Prof.) Tom Ojienda wa Kisumu. Ni kweli kwamba hapa Kenya, hususan pande za Kisumu na maeneo ya Nyando, hutatizwa sana na mafuriko. Zaidi sana wananchi hupoteza maisha yao. Bw. Spika, tukizingatia vile vile hali ya mafuriko, wakati wa mvua ukifika hakuna hata siku moja tumeweza kuona Serikali yetu ya Kenya Kwanza ikiweka kipaumbele mambo ya mafuriko. Kitu tunaona tu ni kwamba wananchi wengi wanasombwa na maji wakati wa mafuriko, wengine wanafariki na hata wengine kutolewa katika maeneo ambayo yako chini kule walikoweza kujisitiri kiamaisha kama nyumbani The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}