GET /api/v0.1/hansard/entries/1545074/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1545074,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545074/?format=api",
"text_counter": 124,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "kwao. Hatimaye wale watu wetu wakaweza kuchukuliwa na kuwekwa katika maeneo ambayo yako juu kidogo na mto huko chini. Miaka mitano hivi ama sita, nakumbuka kwetu katika Kaunti ya Kilifi pia tulikuwa na janga hili la mafuriko. Wakati mwingi tukipatikana na janga kama hili, inakuwa shida. Watoto na kina mama na wazee ndio wanapata taabu. Hii ni kwa sababu maeneo wanapoishi na kuita nyumbani yanasombwa na maji. Mifugo na hata kuku wanachukuliwa na maji na wanaenda, halafu hasara inakuwa kubwa sana. Bw. Spika, ingekuwa vyema ikiwa Serikali inaweza kujiandaa na kujitayarisha vizuri wakati huu ambao mafuriko yanatarajiwa kuja. Ukienda upande wa Bunyala, utaona kila mwaka ujao na uchao, kila tukiendelea mafuriko kule yanaua watu na kufurika maeneo fulani. Kwa hivyo, katika Taarifa hii ningependa sana maeneo yote katika nchi ya Kenya kuchunguzwa ili kuonekana kule ambako kuna uwezekano kuwa na mafuriko ambayo yanaweza kuletea wananchi taabu, kuwaondoa manyumbani kwao na hata kupoteza mifugo yao. Wakati mwingine makaburi yanaoshwa na mafuriko. Kwa hiyo, kuna umuhimu wa Serikali kujiandaa ili izingatie mambo ya mafuriko msimu unaokuja wa mvua. Asante, Bw. Spika."
}