GET /api/v0.1/hansard/entries/1545115/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1545115,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545115/?format=api",
"text_counter": 165,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Mjadala wa Ripoti ya Kamati ya Fedha na Bugeti ya Bunge hili kuhusiana na mipango ya kuthibiti madeni katika mwaka 2025/2026. Hatuna habari nzuri kuhusiana na deni katika nchi yetu kwa sababu, deni limepanda kutoka trilioni kumi nukta mbili tokea Juni mwaka jana mpaka trilioni kumi na moja kufikia Januari thelathini na moja mwaka huu. Deni hili limeongezeka likiwa ni pamoja na deni la nyumbani la karibu trilioni tano nukta sita na deni la kimataifa la kutoka nchi za inje ambalo ni trilioni tano nukta nne. Katika mipango kama hii iliyoletwa mwaka jana, Hazina Kuu walikuwa wamependekeza kwamba ijapokuwa deni limepita kile kiwango kinachostahili, yaani asili mia hamsini na tano ya mapato ya nchi, wanayo mipango ya kuipunguza polepole kufikia mwaka 2027 deni hili litakuwa limefika katika kiwango cha asili mia hamsini na tano ambacho ndicho sheria ambayo tuliipitisha mwaka juzi inanavyosema kuhusiana na deni ambalo liko nchini. Mwelekeo ni kuwa hivi viwango vya deni hili havitapungua mpaka mwaka 2030. Na kwa sababu hiyo ndiyo kuletwa Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Fedha (Public Finance Management Act). Kuna mapendekezo ya kuibadilisha ili ule muhula wa kuhudumu uanze wakati sheria itakapobadilishwa kuliko vile tulipitisha mwaka 2023. Kwa sababu hiyo, tunaendelea kuchukua deni na deni na jambo hili litaweza kuathiri vizazi vijavyo. Deni hii ambayo tunaichukuwa sasa, mara nyingine hata Hazina Kuu haiwezi kueleza pesa zile zimetumika kivipi. Kwa mfano, jana tulipokuwa na mkutano wa Kamati ya Fedha na Bajeti, Waziri John Mbadi aliielezea kamati kwamba mnamo tahere 22.8.2022 kulichukuliwa deni. Kabla ya Serikali hii kuingia mamlaka, kulichukuliwa deni la bilioni kadhaa, nafikiri ni shilingi bilioni kumi na moja. Waziri, hakuweza kueleza deni hii ilitumika kwa mambo gani katika nchi yetu. Kwa hivyo, deni zinachukuliwa lakini hatuoni miradi yoyote ya kiserikali ambayo inafanyika. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}