GET /api/v0.1/hansard/entries/1545116/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1545116,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545116/?format=api",
    "text_counter": 166,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Vile vile, kuna madeni ambayo yamechukuliwa lakini miradi haijaanza. Asubuhi ya leo Waziri wa Maji, Usafi wa Mazingira na Unyunyuziaji alisema hakuna pesa za kulipa ridhaa kwa wale ambao ardhi zao zinachukuliwa kwa hizo miradi za maji. Ukiangalia katika Wizara ya Barabara na Uchukuzi, kuna miradi mingi ambayo imeanzishwa kupitia kwa ufadhili wa wahisani wetu lakini Serikali haijalipa ridhaa wale ambao ardhi zao zinachukuliwa ili barabara hizo zijengwe. Takriban Shilingi bilioni mia mbili zinahitajika kulipa ridhaa kwa wale ambao ardhi zao zinachukuliwa ili miradi hiyo iweze kufanywa. Kwa hivyo, utapata kuwa pesa zimekopwa na zimekaa katika account lakini hakuna kitu ambacho kinafanyika. Pesa ziko katika benki lakini hakuna mradi unaoendelea kwa sababu serikali haijaweza kuwalipa ridhaa wale ambao ardhi zao zimeadhiriwa na miradi hiyo. Vile vile, kuna zile pesa ambazo zinalipwa na Serikali kama commitment fee. Pesa hizi zinalipwa lakini hakuna kitu ambacho kinafanyika. Kwa hivyo, tunaendelea kulipa madeni ilhali hiyo miradi ambayo inatakikana kufanyika, na iliyofadhiliwa na pesa hizo haijafanyika na kuonekana kuna mazao yanapatikana katika miradi hiyo. Mhe. Spika, jambo lingine ni kuwa Serikali inavyokopa ndivyo ambavyo inazuia wafanyi biashara nchini kwetu kukopa na kufanya biashara zao na kupata faida ili waendelee kulipa kodi. Ikiwa serikali inashindana na wafanyi biashara katika mabenki kukopa pesa, serikali itakopa zaidi kuliko wafanyi biashara kwa sababu serikali iko na s ecurity ama idhibati ya kutosha kuhakikisha kwamba huo mkopo utalipwa. Hata hivyo, kuna wale ambao wanakopa kama wafanyi biashara wa kibinafsi. Wengine wamechukuwa mikopo kufanya miradi ya county. Hivi sasa, serikali za county hazilipi. Vile vile, wengine wamechukua mikopo kufanya mikopo ya serikali kuu, ilhali Serikali Kuu hailipi hayo madeni. Kwa hivyo, ufadhili katika benki hizi utapendelea zaidi wachukue mikopo ya serikali kwa sababu wana uhakika kwamba deni zao zitalipwa, kuliko mtu binafsi ambaye ni mfanyi biashara na hivyo basi biashara zitakufa na hatutaweza kukusanya kodi ya kutosha ya kulipia mikopo hizi. Mhe. Spika, jambo la mwisho ambalo ningependa kuzungumzia ni kwamba, ijapokuwa Serikali Kuu ina nafasi ya kukopa, serikali za kaunti hazina nafasi kama hiyo ya kukopa. Ikiwa atataka kukopa lazima apitie kwa Hazina Kuu na kupata ruhusa ya kukopa, huku mara nyingi ikiwa ni shida kukopa. Kwa hivyo, tunasema kuwa, kwanza Serikali lazima ipunguze matumizi yake. Si lazima wajenge masoko au nyumba za wastani ili wananchi wapate nyumba hizo, yaani affordable housing . Si lazima tufanye sasa. Kwa sababu Uchumi wetu hauwezi kubeba miradi hiyo yote na tuweze kupata maendeleo ambayo itatuwezesha kusonga mbele. Mhe. Spika, tukiangalia katika sehemu nyingi, miradi hii ya affordable housing imekwama, kwa sababu ya ukosefu wa pesa. Hata wengi wa wale wafanyi biashara wa kibinafsi ambao waliekeza katika miradi hii wameshindwa kuuza nyumba hizo kwa sababu hakuna pesa mifukoni mwa Wakenya. Wakenya wengi hawawezi kudhibiti malipo ambayo yanatakikana kulipiwa kila mwezi au kila mara kwa mara ili waweze kuziweka nyumba hizo. Mhe. Spika, kuanza Jumatatu, Jumanne, labda hadi Jumatano, kuna kurasa zaidi ya kumi katika magazeti ambazo zinaonyesha kwamba mali ya Wakenya inauzwa kwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}