GET /api/v0.1/hansard/entries/1545117/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1545117,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545117/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "sababu ya ukosefu wa kulipa madeni ambayo wanachukuwa. Kwa hivyo, hakuna haja ya kujenga nyumba hizi halafu zibaki mahame, na mwishowe popo na wanyama wengine wahamie ndani na kuishi katika nyumba hizi ilhali Wakenya hawawezi kumiliki hizo nyumba. Mhe. Spika, Serikali Kuu inaingilia kazi za kaunti. Unaskia kunajengwa soko na serikali kuu Mjini Mombasa, ilhali soko ile inapaswa kujengwa na Kaunti ya Mombasa. Kilifi wanajengewa masoko na ardhi za kaunti zinachukuliwa na Serikali Kuu kujengwa miradi ambayo serikali za kaunti zinaweza kufanya. Tulipata experience kama hii wakati Serikali Kuu ilipokuja kujenga Mama Ngina Water Front. Walisema sisi tutajenga halafu tutaipeana kwa Serikali ya Kaunti ya Mombasa. Wakati huo Waziri wa Utalii alikuwa Mhe. Balala. Baadaye, title deed ya Mama Ngina Water Front ilipotoka ilipelekwa National Treasury kwa sababu imeekeza katika mradi ule wa Mama Ngina Water Front. Title deed sasa imetoka na imerudi tena katika ofisi ya Gender . Sasa tunapelekwa huku na kule kama kupiga mpira, wakati tunadai haki hiyo. Kwa hivyo, miradi hii yote ambayo Serikali Kuu inapanga kufanya, inafaa ifanywe na serikali za kaunti. Kama kuna pesa za kufanya miradi hii haiwezekani kwamba upande mmoja wanazuia pesa kuja kwenye kaunti. Tulipigana hapa katika kujadili Division of Revenue mpaka tukaenda medition kwa sababu Serikali ilikuwa haina pesa za kutosha. Walituongezea shilingi bilioni tano peke yake kwa zile ambazo walikuwa wamepanga kupeleka katika kaunti zetu. Naona mwaka ufuatao kutakuwa na mvutano sana kwa sababu Kamati yetu ya Fedha na Bajeti imependekeza bilioni mia nne na sitini na tano. Hapo kutakuwa na mvutano kwa sababu Serikali Kuu haiko tayari kupeleka pesa hizo katika kaunti. Hata hivyo, tukiangalia miradi ambayo serikali kuu inataka kufanya, kama vile masoko na nyumba, pesa hizi zikikusanywa pamoja ni nyingi kuliko zile ambazo tumependekeza zipelekwe katika kaunti zetu kama mgao wa 2025/2026. Kwa kumalizia, naunga mkono hii ripoti ambayo imeletwa na Kamati yetu ya Fedha na Bajeti. Tujaribu kuhakikisha ya kwamba tunaiweka Serikali mahali pake kwa maswala ya mikopo. Kuna mikopo mingi ambayo inachukuliwa. Tulipofungua Bunge, niliona ripoti ya madeni ya nchi ililetwa lakini hatujapata fursa ya kuijadili kwa sababu tulikuwa tunajadiliana na maswala ya Budget Policy Statement pamoja na Medium-Term Debt Management Strategy. Lakini, baada ya hapo tutaingilia maswala hayo ya deni kwa sababu deni ndiyo inatukwaza zaidi sisi Wakenya katika kupata maendeleo ambayo tunastahili kupata katika nchi yetu. Asante, Mhe. Spika, kwa kunipa fursa hii."
}