GET /api/v0.1/hansard/entries/1545362/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1545362,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545362/?format=api",
"text_counter": 147,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Mtahiki Spika. Ningependa kuuliza Mhe. Waziri swali moja. Kuna sehemu kubwa sana ya shamba ambalo wanajeshi wa Mariakani Army Barracks wamelichukua na wanaishi humo. Familia husika zilitupwa nje. Wamejaribu sana kupata ardhi yao lakini mpaka sasa hawajawahi kuipata. Je, Wizara yako imechukua hatua gani kuona ya kwamba shamba hili ambalo familia nyingi zilidhulumiwa zimerejeshewa? Wananchi hawawezi kufanya chochote kwa sababu ni wanajeshi wanakaa katika ardhi hiyo. Nina uhakika ya kwamba unajua kuwa kikosi cha jeshi kilipoenda pale, kulikuwa wananchi wakiishi pale. Ni hatua gani umechukua kuona kwamba shamba hilo limerudi kwa wakaazi wale au wenye shamba hilo?"
}