GET /api/v0.1/hansard/entries/1545550/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1545550,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545550/?format=api",
"text_counter": 105,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii ili nitoe maoni yangu kuhusu chanjo za mifugo. Sisi watu wa Kaunti ya Tana River tumekuwa na wasiwasi kwa sababu tangu chanjo hii itangazwe na Serikali Kuu, kumeingia mushkil. Wengine wanasema zina shida na wengine wanasema ziko sawa. Tungependa Kamati husika iangalie na iseme kwa kikamilifu kwamba hizi chanjo ni safi na zitatusaidia pamoja na mifugo wetu. Pili, wanafaa kutueleza ni pesa ngapi zinatumika kwa mpango huu wa Serikali. Je hii pesa inatoka kwenye Serikali ya Kenya au kwa wafadhili yaani donors ? Swali la tatu na la mwisho, je, ni bajeti ya pesa ngapi ambayo Kaunti ya Tana River imeweka kwa minajili ya kuchanja mifugo yetu haswa wakati huu tunapoenda msimu wa mvua? Bw. Spika ningependa kamati ichunguze maswala haya ili tujue ukweli wa mambo. Watu wanataka kujua ukweli kabisa. Ikiwezekana Kamati inafaa kuwaongelesha wanasayansi wanaohusika na mambo haya kwa sababu kuna siasa ambayo imeingizwa na wale wanaohusika na sekta ya mifugo wana wasiwasi. Asante."
}