GET /api/v0.1/hansard/entries/1545743/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1545743,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545743/?format=api",
"text_counter": 48,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "ugatuzi. Pesa ambazo zinaenda kwa kaunti hazikuji kwetu kama Maseneta. Pesa hizo zinaenda kufaidi Wakenya. Kwa hivyo, ningetaka kuwasuta kwa hilo na kuwaambia ya kwamba miwa ukipewa kibogoyo mzee kama zawadi, inakuwa ni matusi. Pesa tunazopitisha siku ya leo zimecheleweshwa kwa sababu ya vuta nikuvute ambayo haina maana. Tunafuraha kwa sababu maafisa ambao wanafanya kazi ngumu katika gatuzi zetu watapata pesa zao. Naona Kirinyaga wako na Shilingi 6,000,000. Hakukuwa na maana yoyote ya kuchelewa kulipa wafanyikazi hao kiwango hicho ilhali wanafanya kazi ngumu kule mashinani. Wengi wao wanaenda kazini wakitembea kama mawakala wa ng’ombe. Wengine hawana hata usafiri ya kuhakikisha kwamba afya inatunzwa kule mashinani. Mateso yao yalitokea kwa sababu ya jitihada ambazo zilifanywa na Wabunge wa Bunge la Kitaifa. Walichelewesha Mswada ambao tunapitisha hapa. Tumepewa kazi moja muhimu; kuwa walinzi wa ugatuzi. Lakini, mlinzi pia lazima apewe silaha. Bunge la Seneti limebweka ya kutosha. Wakati wa kuuma umefika. Tukifanya hivyo, watajua ya kwamba hata sisi sio vikaragosi na wanasesere wa siasa. Wanafaa kujua ya kwamba sisi ni Seneti na tuko na jukumu ambalo tumepewa na lazima tufanye. Kuna vile wanatuchukulia virahisi kama bei ya chumvi. Hii ni kwa sababu hao hupinga Mswada wowote ambao tumepeleka kule. Unatapa ya kwamba hata wale ambao hawajasoma wanaongea mitaani na kupinga ule Mswada. Lazima tufanye jitihada ili tueleweke na tuheshimike. Jambo la kushangaza sana ni kwamba vita vimekuja kwa sababu ya pesa ambazo zinafaa kwenda kuangalia maswala ya barabara mashinani. Hao wanajua ya kwamba kuna zile barabara ambazo zinashughulikiwa na Kenya National Highways Authority (KeNHA), Kenya Rural Roads Authority (KeRRA), Kenya Urban Roads Authority (KURA) na zile ambazo zinashughulikiwa na kaunti zetu. Walitoa pesa ambazo zinafaa kwenda kuangalia masuala ya barabara na hatua hiyo imefanya barabara katika kaunti nyingi kukaa kama mahandaki. Hizo barabara zimechimbika kwa sababu hakuna pesa za kuzitengeneza. Leo, Seneta yeyote ambaye yuko hapa akikutana na gavana wake atapigwa pambaja kwa kazi nzuri. Hii ni kwa sababu tunapitisha pesa ambazo zitaenda mashinani ilhali kesho, tutakuwa maadui wa hao magavana ambao tunatetea siku ya leo. Utasikia wakisema ya kwamba, “anapiga kelele. Hajui kazi yake.” Leo tunajua kazi yetu ilhali kesho watasema ya kwamba hatujui kazi yetu. Tumebweka tukahakikisha ya kwamba magavana wamepata pesa na hivyo ndivyo tutabweka pesa zisipotumika visivyo. Ahsante."
}