GET /api/v0.1/hansard/entries/1545782/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1545782,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545782/?format=api",
    "text_counter": 87,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Mwanzo, ningependa kuunga mkono Mswada huu, na vile vile kupongeza Kamati ya Seneti ya Fedha ana Bajeti amabyo inaongozwa na Sen. Roba, kwa kazi nzuri ambayo wamefanya. Jukumu letu kubwa kama Seneti kulingana na Kipengee 96 cha Katiba, ni ugavi wa pesa ambazo zinaenda katika gatuzi zetu na kutetea na kulinda gatuzi zetu. Kiranja wa Wengi, Sen. (Dkt.) Boni Khalwale, amesema ya kwamba sisi ni maadui wa gatuzi. Ningependa kumkosoa kwa sababu sisi sio maadui. Sisi hutetea na kuzilinga gatuzi zetu dhidi ya maadui zake. Bw. Naibu Spika, napongeza vile ambavyo wauguzi wa nyanjani wamepewa hela. Kwa mfano, nikiangalia kwetu, Kaunti ya Laikipia, naona wamepewa Shilingi milioni 25 kwa sababu hao ndio wanafanya kazi nzuri. Ukitembea nchi ya Cuba, utaona hawa wahudumu wa nyanjani ndio wanahusika pakubwa kuwatibu wananchi mashinani. Mgonjwa awe na ugonjwa wa saratani au moyo na magonjwa mengine ambayo yanawaadhiri watu wetu mashinani, ni wao wako kuwaangalia na kuwashughulikia wagonjwa wetu. Bw. Naibu Spika, ni kero katika nchi yetu kupata kuwa hawajalipwa. Ndiposa wakati huu nashukuru kamati kwa sababu tayari wameweka Shilingi milioni 25 ambazo zitaenda kwa wauguzi wetu wa nyajani katika Kaunti ya Laikipia. Ningependa sana kujadili mambo ya Laikipia kwa sababu kila Seneta ambaye yuko hapa anaweza akaguzia kaunti yake. Ukiangalia swala la kulipa madeni ya maafisa wa afya kwenye gatuzi zetu, Kaunti ya Laikipia imetengewa Shilingi milioni 40. Hii itasaidia kwani hivi juzi ulienda kwenye lango la Seneti kuchukua ombi la madaktari hawa. Kila wakati wako kwenye maandamano kwani hawajapewa pesa yao. Tunategemea wauguzi hawa. Ni muhimu kuelewa kuwa unaweza kosa barabara ama elimu lakini ukiwa mgonjwa unaweza ukafa. Ni vizuri sana vile hela hizi zimetengwa ili wauguzi hawa wapate haki yao."
}