GET /api/v0.1/hansard/entries/1545788/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1545788,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545788/?format=api",
"text_counter": 93,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Kaunti ya Laikipia tunakuza nyanya na sisi ni wakulima wa mifugo. Itatubidi tuchague ni kipi ambacho tutaongeza dhamana. Kaunti ya Uasin Gishu wajue ni bidhaa gani wataongeza dhamana ili tusifanye jambo moja sisi wote. Pia kaunti ya Narok inaweza chagua kama ni ng’ombe ama maziwa. Tunashabikia Narok wafanye ile kazi. Kaunti ya Nyamira unapata ni mandizi inaongezwa dhamana. Lakini isiwe ukienda kwenye Kaunti ya Narok, Kisii na Nyamira wote wanaongeza maziwa dhamana. Hii itakuwa ni kazi bure. Lazima tujipange ili tujue ni kaunti ipi itafanya nini."
}