GET /api/v0.1/hansard/entries/1545789/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1545789,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545789/?format=api",
    "text_counter": 94,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Naunga mkono RMLF. Barabara zigawanywa vizuri kama za gatuzi na Serikali kuu. Pia gatuzi zetu zinahitaji zile pesa. Hivi juzi Waziri wa Barabara alikuja na kutuambia kwamba shillingi saba zitatumika kulipa madeni ya Serikali kuu. Lakini hata gatuzi zetu zina madeni. Sisi Wakenya tumetoa shillingi saba kama ushuru wa mafuta tukinunua. Pesa hizi zinafaa kaunti zipate mgao wao. Nikiangalia katika ratiba ya pili, Kaunti ya Laikipia kulingana na ugavi wa fedha hizi za RLMF, tungepewa shillingi millioni 235. Naomba korti zetu ziharakishe kusikiliza kesi hii ili tupate mgao huu. Nitasimama kidete kwa sababu barabara za Laikipi ziko hali mbaya. Bunge la Taifa linaleta mzozo huu ili kaunti zetu zisipate hela hizi. Tutapinga jambo hili leo, kesho, kesho kutwa, mtondo na mtondogoo. Shillingi million 235 zitakazo tengwa kwenda Kaunti ya Laikipia, tusiambie kuwa eti gavana atatumia pesa hizi vibaya. Kuna sheria zitafuatwa. Akitumia pesa vibaya, kuna kamati ambayo inaongozwa na Sen. M. Kajwang’ na nyingine ambayo inaongozwa na Sen. Osotsi ambazo zinaangalia matumizi ya pesa kwa undani katika kaunti zetu. Bw. Naibu Spika, tuna wawakilishi wadi ambao hufanya oversight. Pesa zikose kupelekwa katika kaunti kwa sababu ya wizi. Nani alisema Wabunge wa Bunge la Kitaifa ni malaika? Sisi tunapendekeza kwamba pesa hizi zifike katika gatuzi zetu. Katika ratiba ya kwanza kuna makao makuu ya gatuzi zetu ambayo pesa za ujenzi zimetengwa ili makao haya yamalizike. Inasemekana ni makao makuu ya kaunti tano lakini nikiangalia mswada naona ni kaunti nne. Kuna Isiolo, Lamu, Tana River na Tharaka-Nithi. Sijui ya tano ni ipi kwani haiko hapa. Lazima tuwe na marekebisho ili tuongeze pesa ya Nyandarua kwani wanahitaji makao makuu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}