GET /api/v0.1/hansard/entries/1545942/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1545942,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545942/?format=api",
"text_counter": 45,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa hii fursa umenipa ili kuunga mkono Hoja ya kuidhinisha Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Uhasibu wa Fedha za Umma katika Kaunti. Majukumu ya Seneti imenukuliwa katika Ibara ya 96 ya Katiba ya Kenya. Ibara hii inasema kuwa kazi yetu ni kulinda magatuzi. Katika hekima ya waliotunga Katiba yetu mwaka wa 2010 kuna viwango viwili vya serikali, Serikali za Kaunti na Serikali Kuu. Seneti ikapewa jukumu la kupitisha sheria ya ugavi wa pesa kwa magatuzi. Sheria hii ya ugavi wa pesa kati ya Serikali Kuu na kaunti inaitwa Division of Revenue Act. Pia tulipitisha sheria inayogawanya fedha kwa kaunti 47 inayoitwa County Allocation of Revenue Act. Leo katika hiki kikao maalum tumejadili asubuhi ili kuongeza pesa zaidi ya shillingi billioni 50 kwa gatuzi zetu. Pesa hizi zinaitwa conditional grants. Pesa zikifika kwenye gatuzi wale wanaofanya bajeti ni wafanyikazi wa kaunti kwenye Executive pamoja na Bunge za Magatuzi ama county assemblies. Pia wanajukumu la kutekeleza miradi. Wakati wa kutekeleza miradi kamati za Bunge za kaunti inatakikana kufuatilia miradi hii. Katika uangalizi ama oversight Bunge kwenye kaunti inafaa kufuatilia miradi ifanyike kulingana na sheria, bajeti na uamuzi wa wananchi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}