GET /api/v0.1/hansard/entries/1545943/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1545943,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545943/?format=api",
"text_counter": 46,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Mhasibu mkuu anajukumu ya kwenda kwenye kaunti na kuangalia kama pesa zimetumika vizuri. Ibara ya 229 ya Katiba, inaashiria kuwa mhasibu amalize uhasibu wake na kutoa ripoti kufikia Disemba 31 na kuleta ripoti hizi kwenye Bunge. Mhasibu ameleta ripoti zake katika Bunge la Seneti na pia amezipeleka katika mabunge 47 ya gatuzi nchini. Ibara ya 179(4) inakubalia Seneti iitishe ripoti kutoka kwa magavana ambao ni wakurugenzi wakuu ama CEOs kuja katika Kamati na kujibu maswali. Kamati ya Seneti ambayo mimi ni naibu mwenyekiti iliandikia gatuzi zote 47 ambazo ni watendakazi na bunge zao na wakaleta majibu yao. Katika Ibara ya 201 inatakikana kuwa kila gatuzi litumie pesa katika hali ya uwazi. Tukiita magavana walete ripoti za matumizi ya pesa, tunataka kuhakikisha kwamba pesa zinazoenda kwa gatuzi zetu zimetumika kulingana na sheria. Pia kusaidia yule Mkenya aliye kwenye gatuzi kupata huduma zinazofaa. Vile mwenyekiti wangu ametangulia kusema ni kwamba kuna gatuzi kadhaa ambazo hawakuitika mwito wa kuja mbele ya kamati yetu ya Seneti ili kujibu maswali haya. Kaunti hizi ni Isiolo, Kiambu, Baringo, Marsabit, Nyamira na Kajiado. Gatuzi hizi zilipewa fursa nyingine ili kuja kujibu maswali ya matumizi ya pesa. Ripoti ambazo ziko mbele ya Bunge hii ni tatu. Ripoti ya kwanza ni ya County Executives nay a pili ni ya County Assemblies. Ya tatu ni ripoti ya uaminifu ambayo Bw. Mwenyekiti ameiita Fiduciary Report. Kwa Kiswahili hii ni ripoti ya uaminifu. Tumepitia hizi ripoti zote na kuna masuala kadhaa ambayo imetangulia kujadiliwa tayari ambayo yanaashiria kwamba pesa na mali ya umma katika magatuzi haiko kwenye hali nzuri. Suala la kwanza ni ukosefu wa nakala ya mali na raslimali za gatuzi zetu. Kwa kimombo tunaiita asset register. Wakati nakala ya mali ya gatuzi zetu isipokuwepo, kuna uwezekano wa gatuzi kupoteza mali yao. Kwa mfano, ripoti ya magari mangapi yaliyo katika gatuzi zetu, ripoti ya mashamba yaliyo katika gatuzi zetu. Ni mashamba mangapi hayana hati miliki. Kuna uwezekano wa mashamba haya kupotea kwa sababu hakuna hati miliki kuonyesha kwamba mali hii ni ya kaunti. Jambo lingine ambalo linaashiria kupoteza kwa pesa kulingana na ripoti ya uaminifu ni shida ya kukusanya ushuru wa magatuzi. Gatuzi nyingi zinakusanya ushuru na hazipeleki pesa hizi katika hazina zao. Kaunti nyingi hutumia ushuru baada ya kukusanya ilhali sheria inasema kuwa wakati ushuru umekusanywa upelekwe kwa County Revenue Fund Account. Ushuru utatumika baada ya kufanyiwa bajeti pamoja na pesa zinazotoka kwenye hazina ya kitaifa. Wengine pia wanakusanya ushuru bila kutumia utandawazi. Wakati ushuru unakusanywa bila utandawazi, pesa nyingi hupotea kulingana na ripoti hii ya Mhasibu Mkuu."
}