GET /api/v0.1/hansard/entries/1545953/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1545953,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545953/?format=api",
"text_counter": 56,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "kwa gatuzi zetu kwa sababu pesa ikienda huko inaenda kutumika vibaya. Nani hajui ya kwamba ufisadi mwingi uko katika maeneo bunge. Waheshimiwa wengi Wabunge wanafanya tender zao wenyewe. Nilikuwa mahali nikiongea na wananchi katika hadhara na mambo yangu ya uangalizi. Wananchi wanauliza inawezekanaje mheshimiwa siku hizi barabara zikitengenezwa zikiwekwa simiti zinakaa mwaka mmoja na kuharibika. Zamani barabara zilikuwa zinatengenezwa na kukaa kama miaka kumi na tano. Nikawaambia ni kwa sababu ya ufisadi na ulafi wa Wabunge. Wale Wabunge wanafanya tender zao wenyewe. Na kama hawajafanya tender zao wenyewe, ule ufisadi wa kuitisha hongo unakuwa mwingi sana. Sasa kama mwanakandarasi atakupatia hongo ya asilimia 20, ni lazima aweke simiti kidogo na mchanga mwingi. Kwa hivyo, unapata barabara imetengenezwa na baada ya mwaka mmoja imetoa waya tayari."
}