GET /api/v0.1/hansard/entries/1545998/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1545998,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545998/?format=api",
    "text_counter": 101,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kuna mambo ya nyumba ambazo zimejengwa, kuna jambo linalohusu CHPs ili wapate pesa. Kuna mambo ya barabara na kaunti zimewasilisha kesi kortini. Kama mahakama itakubaliana nao, Kaunti ya Embu inastahili kupata Shilingi 211milioni. Wadi zote zitafaidika na hizi pesa. Wakati huu mvua inanyesha, magari yanakwama. Naomba mahakama iweze kutusaidia. Bw. Naibu Spika, mimi ninaomba mahakama iweze kusaidia ndiposa magavana waweze kupata pesa inayofaa. Wabunge wa Bunge la Kitaifa wote wako na pesa. Wako na pesa ya National Government Constituencies Development Fund (NG-CDF), pesa ya barabara na bado wako na pesa ya sitima. Wako na hizo pesa zote lakini hakuna mtu anaangalia matumizi ya pesa hizo. Ningeomba kwamba hata kama tunafuata pesa kwa ajili ya magavana wetu kufanya kazi yao, hata Seneti inahitaji kupewa nguvu ya kufanya kazi ya oversight vizuri. Maseneta wakifanya kazi vizuri, magavana watahakikisha ya kwamba pesa zile ambazo wamepewa zimetumika kwa njia inayofaa. Wajumbe wote ni lazima wakubali kusaidia kaunti ili waipate pesa. Tuko hapa kama Maseneta kuongea mambo ya ugatuzi na matatizo ambayo magavana wanapata. Ninaunga mkono kazi ambayo imefanywa na kamati hizi mbili. Asante."
}