GET /api/v0.1/hansard/entries/1546253/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1546253,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1546253/?format=api",
"text_counter": 22,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaloleni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Paul Katana",
"speaker": null,
"content": " Asante, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipatia nafasi hii kuchangia kuhusu ardhi hii. Wakaazi kuhangaishwa na masuala ya mashamba yamezidi sana, hasa sehemu za Pwani. Utakuta watu wamekaa katika mashamba yao kwa muda mrefu sana, lakini kwa sababu ya uzembe wa baadhi ya maafisa wa Serikali ambao wametwikwa jukumu la kusaidia wananchi kupata hatimiliki, wamekuwa chanzo cha kusaidia mabwenyenye na watu ambao hawana uhusiano na mashamba hayo na utamaduni wa pale. Wanawapatia hatimiliki kinyume na matarajio ya wananchi hao. La kutamausha zaidi ni kwamba hata polisi wanaingilia sana mambo ya mashamba kuliko kulinda usalama wa wananchi. Wanapewa amri ya kortini lakini hawadhibitishi. Usiku wanahangaisha wananchi na kuvunja nyumba zao, wakisema shamba ni la mtu fulani, bila kuhusisha taasisi zinazohusika kama NLC na Wizara ya Ardhi. Kwa hivyo, ninaunga mkono kuwa ardhi hii iangaliwe vizuri ili hawa wananchi wapate haki yao. Kumekuwa na visa vingi sana hasa sehemu za Pwani. Kuna wananchi ambao wamekaa kwa mashamba ya mababu zao, mahali kuna makaburi yao, makanisa, misikiti na mashule, lakini mtu anakuja na kusema shamba ni lake. Tunaomba haya masuala ya uskwota katika The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}