GET /api/v0.1/hansard/entries/1546270/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1546270,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1546270/?format=api",
"text_counter": 39,
"type": "speech",
"speaker_name": "Emgwen, UDA",
"speaker_title": "Hon. Josses Lelmengit",
"speaker": null,
"content": " Asante sana Mhe. Naibu wa Spika. Ningependa kuchangia petition hii kutoka kwa Mheshimiwa wa Pwani, Mhe. Ken Chonga. Swala la land grabbing haliko tu sehemu ya Pwani pekee yake bali liko katika sehemu zote Kenya. Nikiwa mmoja wa Mjumbe wa Departmental Committee on Lands, mimi husikitika sana na kuhisi uchungu sana wakati ambapo wazee wanakuja katika kikao chetu na malalamishi ya shamba kuwa watu wamewanyang’anya shamba. Huja wakilia kuwa maswala hayo hayajatatuliwa takriban zaidi ya miaka 30. Ni uchungu sana. Ingawa tuko na mikakati na sheria ambazo zinahusu masuala ya umiliki wa mashamba, imekuwa shida sana. Licha ya Waziri na Katibu wake kuweka mikakati hio, haitoshi. Nasihi Wizara ya Interior and Coordination of National Government na Kamati ya Public Petitions kushirikiana na kuexpidite hii process, ili walionyang’anywa mashamba wapate haki na waishi kwa amani."
}