GET /api/v0.1/hansard/entries/1546361/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1546361,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1546361/?format=api",
"text_counter": 130,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Kwanza nataka kuwaambia watu wangu wa Mombasa kuwa hawakuniona maana nilikuwa katika likizo ya miezi miwili nikiugua. Sasa mimerudi. Wataniona Bunge nikichapa kazi. Nachukua fursa hii kumpongeza Mhe. Atandi kwa kuleta Mswada huu unaosisitiza tuwe na viwanda vyetu vya mbolea ili tuboresha ukulima katika taifa hili. Tuongeze viwanda vyetu vya kutengeneza mbolea. Tunaagiza mbolea kutoka mataifa ya nje kwa sababu viwanda vyetu havitoshelezi wakulima wote. Kwa hivyo, Serikali ikiwekeza kwa ujenzi wa viwanda vya mbolea itatuletea faida kubwa. Vijana wetu watapata ajira. Tunavyojua, wakati huu na wakati wa Corona, vijana wengi walipoteza kazi na nafasi za kazi zimekuwa haba. Tukiongeza viwanda vya kutengeneza mbolea, vitatoa nafasi za ajira kwa vijana katika taifa letu. Mwaka jana, Mhe. Naibu Spika, dada yetu Gladys Sholei alileta Mswada kuhusu mbolea za sumu zilizokuwa zikiingia katika taifa hili. Wakulima walikuwa wakizitumia bila The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}