GET /api/v0.1/hansard/entries/1546362/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1546362,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1546362/?format=api",
    "text_counter": 131,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "kujua. Ziliwaletea maradhi mengi ya kutamausha kama vile kansa. Katika ubora wa bidhaa, tuwe na viwanda vyetu Kenya ambavyo vitaweza kufanya uchunguzi wa kutosha ili wakulima wajue mbolea zinazotoka humo ni bora kwa afya na mazingira. Tukiwa na viwanda vyetu vya mbolea, afya yetu na mazingira yatakuwa sawa kwa sababu hivyo viwanda vitaangalia ubora wa bidhaa zao katika taifa letu. Udongo wetu ni tofauti na udongo wa mataifa tunayonunua mbolea. Tukiwa na viwanda vyetu, udongo wetu utaangaliwa jinsi unavyozalisha; ikiongezwa mbolea ipi itakuwa na afadhali katika mazao au italeta madhara gani. Kwa hivyo, viwanda vyetu vitatengeneza mbolea inayoridhiana na udongo wetu. Mhe. Atandi alisema kuwa miaka miwili iliyopita, Kenya ilitumia takriban Ksh50 bilioni kuleta mbolea za bei ya kupungua katika mpango wa subsidy . Mpaka sasa, wakulima wanapanga foleni ya kutafuta mbolea katika National Cereals and Produce Board. Wengine wanakesha ili wapate mbolea kwa bei nafuu. Tukiongeza viwanda vyetu, haya mapeni ambayo tunapeleka mataifa ya nje tutatumia hapa nyumbani kuboresha mbolea yetu na kuiuza kwa bei nafuu kwa sababu ya kuwa na viwanda vya kutosha. Kwa hivyo, tutapunguza bajeti ya kuagiza bidhaa kutoka nje. Tukiagiza bidhaa kutoka nje, tunatumia pesa nyingi katika clearance mipakani pamoja na mambo mengi mengine. Wakati mwingine mbolea hukaa bandarini kwa muda mrefu ikingoja clearance huku wakulima wakisubiri kupata mbolea hiyo. Viwanda vyetu vikiongezwa, wakulima wataweza kuenda kwa kiwanda chochote kununua mbolea ili walime kwa wakati mwafaka. Leo, wakulima wengi wanalalamika kuwa mvua imeanza na wamelima mashamba japo hawawezi kupanda kwa sababu ya ukosefu wa mbolea. Tukiweza kutengeneza mbolea hapa nyumbani, itarahisisha wakulima kupata mbolea kwa wepesi, kulima, na kupanda kwa wakati. Hili litazidisha uchumi wa taifa letu. Ilivyo sasa, tunapeleka pesa nyingi nje ya nchi. Ikiwa tutafanya bajeti yetu na pesa izunguke nchini, faida kubwa itarudi katika taifa letu na tutapunguza maradhi. Kina mama hulazwa mahospitali kwa sababu ya vyakula wanavyokula vilivyo pandwa kwa kutumia mbolea kutoka ng’ambo. Alivyosema Mhe. Gladys Sholei, hivyo ni chanzo cha maradhi hapa Kenya. Ubora wa ardhi yetu umepotea kwa sababu ya mbolea tunazotumia. Zimeharibu mazingira. Maji yanayotoka katika udongo huo na kuingia katika mito yetu inanywewa ilhali ina sumu kwa sababu ya mbolea zinazotumiwa kutoka nje ya taifa letu. Sumu hii hupatikana katika vyakula vyetu tunavyokula. Watu wengi wamepatwa na maradhi na kupoteza maisha kutokana na vyakula hivi. Naunga mkono Hoja hii. Vijana watapata ajira, afya itakuwa bora, vyakula vitakuwa kwa wingi katika taifa na malalamishi yatapungua. Mtu yeyote mwenye njaa lazima atapiga kelele. Hata hivyo, akishiba chakula kizuri kisichoweza kumletea maradhi, atatulia. Katika hospitali zetu, foleni za watu walio na maradhi itokanayo na vyakula vilivyoingia sumu zitapungua. Nampongeza sana Mhe. Atandi kwa kuleta Hoja hii ambayo ni muhimu sana kwa Wakenya. Napendekeza kuwa wakulima waangaliwe vizuri kwa sababu wao ndio watakaotupa lishe bora na kufanya Wakenya wawe na shibe. Tukifungua viwanda vyetu, bei ya mbolea itashuka. Wengi hupanga foleni kule National Cereals and Produce Board kutafuta mbolea kwa sababu mbolea huko ni bei nafuu. Tukifungua viwanda vyetu na tupunguze bei, tutawafanyia nafuu na watalima wakiwa na raha. Mazao yao shambani yatatoka vizuri na Kenya itastawi. Tusemavyo, ukulima ndio uti wa mgongo wa taifa. Wakulima wakiwa na raha, Wakenya pia watakuwa na furaha. Ahsante sana."
}