GET /api/v0.1/hansard/entries/1547187/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1547187,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1547187/?format=api",
"text_counter": 720,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Mhe. Spika. Kwanza, ninataka nisahihishe kuwa mimi ni Mbunge wa Kaloleni na sio Ganze. Mbunge wa Ganze yuko hapa. Mwaka jana, niliuliza swali kuhusu sehemu zilizo na ugumu. Ulitoa mwelekeo wakati huo na ukamwambia Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi alete majibu. Imekuwa zaidi ya miezi sita tangu useme maneno hayo. Eneo Bunge jirani la Ganze limesajiliwa kama sehemu iliyo na ugumu ilhali watu wa Kaloleni na Ganze wanapata shida sawa. Kwa hivyo, Mhe. Spika, Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi anapaswa alichukulie swala hilo umuhimu zaidi kwa sababu watu wetu wanaumia haswa katika sehemu za Kayafungo, Mwana Mwinga, Mariakani na Kaloleni. Ahsante, Mhe. Spika."
}