GET /api/v0.1/hansard/entries/1547318/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1547318,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1547318/?format=api",
"text_counter": 851,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Kwanza, nawapongeza wale ambao walikaa na kuibua Hoja hii ya malalamiko, ambao ukiuangalia, ni kweli kuwa wale ambao wanafanya shughuli ya bobaboda kupitia mtandao wanadhulumiwa haswa na wale wenye mitandao. Ukiangalia masuala yaliyoorodheshwa hapa, wanafanya kazi kupitia mtandao ambao hawana umiliki na haipo Kenya. Wenye mitandao wanaamua pesa ngapi watakazochukua kutoka kwa wenye bodaboda licha ya kwamba mwenye bodaboda ameinunua ama kuikopa deni analotakiwa kulipa. Anasimamia gharama ya ukarabati bila msaada wowote kutoka kwa wenye mitandao ilhali wanachukua fedha wanavyotaka. Mpaka sasa, serikali haijachukua hatua yoyote kuweza kujumuisha wenye mtandao na wanaofanya biashara hii. Ni jukumu la Bunge hili kubuni sheria na kanuni kama wanavyoomba kwamba tuchukue hatua hiyo ili tuwalinde. Tukumbuke kwamba, kama wabunge na kama serikali, ni jukumu letu kuwatetea wananchi na vijana wetu ambao wanajishughulisha na biashara na shughuli nyingine halali. Si jukumu letu kuwatetea wageni mabwenyenye wenye mitandao. Wakati umefika ambapo Bunge linaweza kutengeneza sheria na miundo msingi ya kuona kwamba wenye hii mitandao wanapitia kanuni na sheria tulizoweka ambazo kupitia huu Mswada, Wizara inayohusika haijatekeleza. Hili ni jambo la kuhuzunisha. Tukubali kuwa ni dhuluma Bunge hili likiendelea kuwacha Wizara husika bila kuwapatia mwelekeo wa kuwalinda watu wetu. Kati ya yale ambayo wanalalamikia ni kwamba wenye mitandao wanaweza kuamua, bila sababu yoyote, kuwatoa kwenye mtandao ilhali wakati wanajiandikisha kwenye mtandao huwa wamejua kwamba watapata riziki. Wanajua watapata ajira kupitia huo mtandao. Wizara husika, na hata Bunge, haijafikiria kutunga sheria ama kanuni ili jambo kama hili lisiweze kutokea. Hii Hoja imefika kwa wakati wake. Ni wakati wetu kuchukua hatua kwa sababu Katiba inatupatia nafasi kutengeneza sheria za kutetea watu wetu ili wasidhulumiwe vile ambavyo wanadhulumiwa. Pia, wamezungumzia majukumu ya serikali za ugatuzi. Mpaka sasa, barabara zetu hazitambui kwamba kuna watu wanafanya biashara halali ya bodaboda. Katika barabara, hakuna sehemu ambazo zimetengewa bodaboda kama ambavyo magari ya teksi yametengewa nafasi. Kukiwepo sheria na kanuni, sioni kwa nini wasifanye biashara na wapate fedha nyingi. Kwa mfano, viwanja vyetu vyote vya ndege hapa nchini vina ilani kwamba waendeshaji bodaboda hawaruhusiwi kuingia ndani. Tunajua bodaboda wana jukumu muhimu. Wanawezatoa huduma za haraka ambazo magari ya kawaida hayawezi. Waendeshaji bodaboda wanawezatoa huduma za nafuu hata kwa wale wafanyakazi katika sehemu kama hizi. Sheria zilizoko sasa ni kwamba hawaruhusiwi kuingia sehemu zingine. Wanabaguliwa."
}