GET /api/v0.1/hansard/entries/1547322/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1547322,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1547322/?format=api",
    "text_counter": 855,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunitunuku dakika mbili. Nilikuwa nasisitiza kwamba mara nyingi hata sisi ambao tuko Bungeni husahau kwamba kuna watu ambao wana biashara za chini. Uwezo wao sio ule wa teksi au basi za kawaida. Lakini yale majukumu ambayo wanatekeleza ni muhimu. Kipato wanachopata ni halali, kinawasimamia, na kinaongeza uchumi katika nchi hii yetu. Kwa hivyo, Hoja hii ni ya kuungwa mkono. Kamati husika ilete hizo kanuni tuzipitishe ili waendeshaji bodaboda wafanye biashara zao kwa kutambulika na kunufaika kama wengineo. Asante, Mhe. Spika wa Muda."
}