GET /api/v0.1/hansard/entries/1547381/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1547381,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1547381/?format=api",
"text_counter": 914,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Mhe. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda. Miaka ishirini iliyopita, nilifanya kazi sehemu za Pokot na Turkana kama mhandisi. Inahuzunisha kuwa unaweza kutembea zaidi ya kilomita 20 sehemu hizi bila kuona shule moja. Kwa nini nazungumza kuhusu shule? Sote hapa kama viongozi, tunakubaliana kwamba kitu ambacho kinaweza kusawazisha maisha ya wanadamu ni elimu. Nakumbuka wakati tulipopata uhuru, katika takwimu, jambo lililotiliwa mkazo sana lilikuwa la kuondoa ujinga. Ujinga haukuwa uondolewe kwa bakora, fimbo au bunduki bali, kupitia elimu. Kwa hivyo, naunga mkono Ripoti hii iliyowasilishwa na Kamati. Sehemu ambayo haijasisitizwa na inayoweza kutoa suluhu kwa haya matatizo ni elimu. Ni jambo la kutamausha katika karne hii, kama ilivyotajwa katika Ripoti kuwa kuna familia zaidi ya maelfu ambazo zimefurushwa katika makazi yao. Hii inamaaniasha moja kwa moja kwamba, watoto wa familia hizi hawako shuleni. Ikiwa hali ni hiyo, hata Serikali ikiwapeleka askari na wanajeshi kule ilihali hao vijana wanaofaa kupata elimu na hatimaye kazi, mbadala wangalipo, jambo hili halitaisha. Sikubaliani na pendekezo la askari kusuluhisha jambo hili. Kama Bunge, tuangalie sehemu hizi kwa upekee na tuzipe fedha. Ijapokuwa Serikali zilizotangulia hazikuweza kufanya hivyo, sisi tuzipe fedha ili ziweze kupata elimu bora na ziwe na shule za mabweni. Nilipokuwa nikifanya kazi sehemu hizo, nilibaini kuwa, hata panapojengwa shule za kawaida, hazipati wanafunzi kwa sababu wengi wao huenda malishoni kuchunga mifugo na kutafuta nyasi na maji. Kwa hivyo, tuko na uwezo wa kuzipa sehemu hizi pesa. Tuwe na kitu tunachokiita kwa Kimombo, “affirmative action” upande wa elimu. Katika kilimo, haswa Wizara ya Maji, kama nilivyokuwa nikiishi sehemu hizo na Ripoti isemavyo, matatizo mengi hutokea kwa sababu ya malisho pale wanapotafuta nyasi na maji. Mbona kama Bunge, tusitenge fedha maalum kupitia Wizara ya Maji ili mabwawa na visima vipewe kipaumbele tutatue janga hili? Kama tunavyoona katika Bajeti, wale walio katika Kamati zinazohusika wanapeleka miradi ya maji maeneo bunge yao ambayo hayana mahitaji kama sehemu zilizotajwa. Mhe. Spika wa Muda, kwa hizi dakika ulizonipa, inafika wakati ambao jambo hili sio la kamati; lakini, tujue uhalifu katika sehemu moja ya nchi ni uhalifu katika nchi nzima. Kama ilivyozungumzwa hapa, ni aibu kubwa watoto na jamii za wale viongozi wa kisisasa wanaoishi Nairobi na ambao, watoto wao wanasoma shule nzuri lakini katika roho zao, wanaona ni vyema watumie watoto wa maskini ambao hawana elimu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}