GET /api/v0.1/hansard/entries/1547399/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1547399,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1547399/?format=api",
"text_counter": 932,
"type": "speech",
"speaker_name": "Elgeyo Marakwet County, Independent",
"speaker_title": "Hon. Caroline Ng’elechei",
"speaker": null,
"content": " Shukrani, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipea fursa niichangie hii Hoja. Ninashukuru Kamati ya Usalama ambayo ilichukua hilo jukumu la kutembea katika Kaunti zote sita ambazo ziko Kerio Valley ili kupata kile kinachoendelea huko mashinani. Mara nyingi unapotegemea wanasiasa, utapata kila mtu anaegemea upande wake. Utapata mwanasiasa kutoka West Pokot akisema kwamba wao hawana makosa na kusingizia kaunti zinazo wazingira. Kwa mfano, utapata mimi mwenye kutoka West Pokot nikidai kwamba sisi ni weupe kama pamba lakini majirani wetu ndio wabaya. Tonavyozunguza sasa hivi, tumesumbuliwa sana na wale magaidi wanaoiba mifugo. Hakuna tofaoti yao na wale “terrorists”. Wanakuja kwenye ardhi ya wenyewe, wanahamisha wenyeji, wanachukua na kuharibu mali yao na kuwaua bila huruma. Kuna jambo limetusumbua kwa muda mrefu. Watu wanaposikia kuhusu ukosefu wa usalama maeneo haya, wanasema viongozi waketi chini na wazungumze. Ukifika Elgeyo Marakwet, uliza “Murkutwa massacre” ni nini. Ilikuwa March 2001 ambapo magaidi zaidi ya elfu tatu kutoka Pokot walivamia kijiji kinachoitwa Murkutwa, Elgeyo Marakwet na kuwaua watu zaidi ya hamsini, wakachoma zaidi ya nyumba mia tatu na kuiba mifugo zaidi ya elfu mbili."
}