GET /api/v0.1/hansard/entries/1547400/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1547400,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1547400/?format=api",
"text_counter": 933,
"type": "speech",
"speaker_name": "Elgeyo Marakwet County, Independent",
"speaker_title": "Hon. Caroline Ng’elechei",
"speaker": null,
"content": "Jambo hili limekuwa donda sugu kana kwamba watoto wadogo wanapokua, wanajua kipaumbele katika eneo hilo ni watu kuvamiana na kuuana. Ijapokuwa Serikali inajaribu, ninataka kuomba kile kitu ambacho Mhe. Makilap kutoka Baringo North Constituency amezungumzia, ya disamarment. Silaha zitolewe mikononi mwa watu. iwapo kuna vita au amani, Serikali ihakikishe kuwa hakuna mwananchi ambaye atabaki na silaha mkononi mwake. Je, anatumia silaha hiyo kufanya nini? Mtu anapomiliki bunduki ama risasi nyumbani mwake, anataka kuzitumia kufanya nini? Huwezi kutumia bunduki ama risasi kuchunga ng’ombe wala kufanya jambo lolote. Unapokuwa na silaha hizo, ina maana kuwa unajitayarisha au upo tayari kumtoa uhai mwenzako."
}