GET /api/v0.1/hansard/entries/1547401/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1547401,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1547401/?format=api",
"text_counter": 934,
"type": "speech",
"speaker_name": "Elgeyo Marakwet County, Independent",
"speaker_title": "Hon. Caroline Ng’elechei",
"speaker": null,
"content": "Jambo hili limetuhangaisha. Tumelia ya kutosha. Ninashukuru Serikali ya Mhe. Ruto kwa sababu tangu aingie mamlakani, tumeongezewa NPR, yaani, raia wanaolinda wenzao. Pia, tumeongezewa askari wa jeshi na wa General Service Unit (GSU). Ukitaka kujua hasara iliyoletwa na wizi wa mifugo nchini, kumbuka kuwa yule Mkuu wa Majeshi alifariki akienda kutazama wanajeshi wake katika eneo hilo. Kwa kawaida, wanajeshi hawakai ndani ya nchi. Wanachunga mipaka yetu kutokana na uvamizi wa nchi jirani. Lakini imebidi wabaki nchini ili walinde eneo hilo dhidi ya magaidi."
}